JINSI YA KUSINDIKA JUISI YA NANASI
Mananasi husindikwa kupata bidhaa zifuatazo
• Jamu
• Juisi
• Mananasi makavu
• Vipande vya mananasi
Vifuatavyo ni vifaa vinavyotumika Kusindika mananasi kupata
juisi
• Kisu kisichoshika kutu
• Mashine ya kukamua juisi
• Meza iliyofunikwa kwa bati la aluminiamu.
• Sufuria
• Jiko
• Chujio
• Chupa
• Kipima joto
Malighafi
• Mananasi yaliyokomaa na kuiva vizuri
• Sukari nyeupe
• Maji safi na salama
Jinsi ya kutengeneza
• Chagua mananasi bora yaliyoiva vizuri
• Osha kwa kutumia maji safi na salama
• Menya kwa kisu kikali ili kuondoa maganda
• Kata vipande vidogo na viweke ndani ya mashine ya kukamua
juisi.
• Kamua juisi kwa kutumia mashine
• Chuja kwa kutumia chujio au kitambaa safi.
• Chemsha juisi kwa muda wa dakika 20 kwenye joto la nyuzi 80
hadi 90 za Sentigredi
• Ipua
• Fungasha juisi ikiwa bado ya moto kwenye chupa zilizochemshwa .
• W eka chupa zenye juisi kwenye sufuria
• W eka maji kiasi cha nusu ya kimo cha chupa na chemsha kwa
muda wa dakika 20
• Ipua na acha chupa zipoe
• W eka lebo
• Hifadhi sehemu yenye ubaridi.
Nanasi lenye ukubwa wa kawaida linalokadiriwa kuwa na uzito wa
kilo moja na nusu lina
weza kutoa zaidi ya nusu lita ya juisi .
JUISI ILIYOTENGENEZWA KWA NJIA HII
INAWEZA KUDUMU KWA MUDA WA MIEZI MITANO
Matumizi ya juisi ya nanasi
• Kiburudisho
• Kikata kiu
No comments:
Post a Comment