Monday, 29 August 2016

NUNUA NANASI NA TUMIA KWA MIEZI MITANO

JINSI YA KUSINDIKA JUISI YA NANASI 
Mananasi husindikwa kupata bidhaa zifuatazo
• Jamu
• Juisi
• Mananasi makavu
• Vipande vya mananasi

Vifuatavyo ni vifaa vinavyotumika Kusindika mananasi kupata juisi
• Kisu kisichoshika kutu
• Mashine ya kukamua juisi
• Meza iliyofunikwa kwa bati la aluminiamu.
• Sufuria
• Jiko
• Chujio
• Chupa
• Kipima joto

Malighafi
• Mananasi yaliyokomaa na kuiva vizuri
• Sukari nyeupe
• Maji safi na salama

Jinsi ya kutengeneza
• Chagua mananasi bora yaliyoiva vizuri
• Osha kwa kutumia maji safi na salama
• Menya kwa kisu kikali ili kuondoa maganda
• Kata vipande vidogo na viweke ndani ya mashine ya kukamua juisi.
• Kamua juisi kwa kutumia mashine
• Chuja kwa kutumia chujio au kitambaa safi.
• Chemsha juisi kwa muda wa dakika 20 kwenye joto la nyuzi 80 hadi 90 za Sentigredi
• Ipua
• Fungasha juisi ikiwa bado ya moto kwenye chupa zilizochemshwa .
• W eka chupa zenye juisi kwenye sufuria
• W eka maji kiasi cha nusu ya kimo cha chupa na chemsha kwa muda wa dakika 20
• Ipua na acha chupa zipoe
• W eka lebo
• Hifadhi sehemu yenye ubaridi.
Nanasi lenye ukubwa wa kawaida linalokadiriwa kuwa na uzito wa kilo moja na nusu lina
weza kutoa zaidi ya nusu lita ya juisi .
JUISI ILIYOTENGENEZWA KWA NJIA HII INAWEZA KUDUMU KWA MUDA WA MIEZI MITANO

Matumizi ya juisi ya nanasi
• Kiburudisho
• Kikata kiu


Monday, 22 August 2016

KILIMO CHA KAROTI

          




Karoti ni zao ambalo hulimwa zaidi katika mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Morogoro, Iringa, Mbeya na Kagera. Ndugu msomaji maeneo tajwa hapo juu hulimwa zaidi kwa maana hiyo karoti inaweza kulimwa katika maeneo mengine pia yenye sifa zinazo kalibiana na hiyo mikoa.  hustawi vizuri kwenye sehemu zenye joto la wastani (nyuzi joto 15 hadi 27 za Sentigredi).
Zao hili hutumika kama kiungo katika mapishi ya vyakula mbalimbali. Huweza kutafunwa mbichi au kuchanganywa kwenye kachumbari. Karoti zina vitamin A, C na madini aina ya chuma.
Karoti hupandwa moja kwa moja shambani katika matuta au sesa. Kiasi cha gramu 80 (sawa na vijiko vidogo vya chai 16) kinatosha kupanda eneo la mita za mraba 100. Eka moja huhitaji kilo 3.2 za mbegu.

Hakikisha mbegu unazozipanda zina uwezo wa kuota kwa kuzifikicha. Mbegu zenye uwezo wa kuota hutoa harufu kali unapozifikicha. Zilizopoteza uwezo wa kuota huwa hazitoi harufu yoyote. Ili mbegu ziote haraka ziloweke katika maji kwa muda wa saa 24. Baada ya hapo changanya mbegu hizo na mchanga, kwa kiasi kinacholingana ili kupata mtawanyiko mzuri wa mbegu wakati wa kupanda/kusia.
 Maandalizi ya shamba
Ø Lima shamba kwa trekta, kwa ng’ombe ama kwa jembe la mkono kwa kina cha sentimita 30 hadi 45
Ø Andaa matuta yenye mwinuko na kimo cha sentimita 30-40, na upana wa mita 1 na mita 1.5 kutoka katikati ya tuta na tuta. Tengeneza mifereji midogo ya kusiha mbegu za karoti yenye umbali wa sentimita 15- 20, mifereji minne kwa tuta
Ø Weka mbegu katika chupa ndogo ya mililita 100 na toboa kidogo mfuniko
Ø Sia mbegu katika mifereji ya kupandia kwa kutikisa chupa yenye mbegu
Ø Funika mbegu kwa kutumia mboji au mchanga
Ø Nyunyiza maji ya kutosha
Ø Funika tuta na plastiki nyeusi
Ø Kandamiza plastiki kwa pembeni na kwa mabonge ya udongo ili isipeperushwe na upepo
Ø Mbegu huota baada ya siku 3-5 kutegemea na hali ya hewa
Ø Zingatia kukagua shamba mara tatu kwa siku.
Ø Ondoa plastiki mara moja pindi utakapoona mbegu moja tu iliyoota
Ø Kuchelewa kuondoa plastiki husababisha miche inayoota kufa kwa kuunguzwa na joto lililo katika plastiki
Palizi
Palilia shamba mara kwa mara ili kuhakikisha shamba halina magugu
Magugu hudhibitiwa kwa palizi ya jembe, kung’oa kwa mkono ama matumizi ya viuagugu
Matumizi ya viuatilifu yafanyike kila baada ya wiki mbili
Mbolea
Tumia mbolea ya DAP wakati wa kupanda, CAN ama SA wiki tatu baadaye na kisha tumia NPK wiki sita baada ya kupanda. Matumizi ya mbolea za maji yafanyike kila baada ya wiki mbili kutegemea na mahitaji

Magonjwa:
· Madoajani (Leaf Spot):
Ugonjwa huu husababishwa na ukungu na hutokea wakati karoti zina urefu wa sentimita 13 mpaka 15. Hushambulia majani na kuyafanya yawe na madoa yenye rangi nyeusi iliyochanganyika na kijivu au kahawia. Sehemu zinazozunguka madoa haya hubadilika rangi na kuwa njano. Ugonjwa ukizidi majani hukauka. Zuia ugonjwa huu kwa kunyunyizia dawa za ukungu kama vile Dithane-M 45, Blitox, Copperhydroxide (Kocide), Copper Oxychloride, Cupric Hydroxide (Champion), Antrocol, Topsin M- 70% na Ridomil.
· Kuoza Mizizi (Sclerotinia Rot).
Ugonjwa huu husababishwa na ukungu na hushambulia mizizi namajani. Dalili zake ni kuoza kwa mizizi na majani. Baadaye sehemu hizi hufunikwa na uyoga mweupe. Kwenye uyoga huu huota siklerotia kubwa zenye rangi nyeusi.
Zuia ugonjwa huu kwa kuzingatia yafuatayo:-
- Epuka kustawisha karoti kwenye maeneo yaliyoshambuliwa na ugonjwa huu.
- Nyunyuzia dawa za ukungu kama vile Dithane M- 45, Blitox, Topsin - M 70% na Ridomil.
· Madoa Meusi (Black Leaf Spot):
Huu pia ni ugonjwa wa ukungu unaoshambulia majani na mizizi. Majani yaliyoshambuliwa huwa na rangi ya manjano ambayo baadaye hubadilika na kuwa kahawia. Mizizi huwa na madoa meusi yaliyodidimia. Ugonjwa huu unaweza kuzuiwa kwa kutumia mbegu zilizothibitishwa kitaalamu, kubadilisha mazao na kuepuka kujeruhi karoti wakati wa kupalilia, kuvuna au kusafirisha.
Wadudu:
· Minyoo Fundo:
Minyoo hii hushambulia mizizi na kuifanya iwe na vinundu. Hali hii husababisha mmea kudumaa na kupunguza mavuno. Minyoo fundo huweza kuzuiwa kwa kubalidilisha mazao. Baada ya kuvuna usipande mazao yajamii ya karoti au mazao yanayoshambuliwa na wadudu hawa. Unawezakupandamazao ambayo bayashambuliwi na minyoo fundo kama vile mahindi. Pia hakikisha shamba ni safi wakati wote.
· Imi wa Karoti:
Mashambulizi hufanywa na funza ambaye hutoboa mizizi. Ili kuzuia wadudu hawa tumia dawa kama vile Dichlorvos, Sapa Diazinon na Fenvalerate. Pia badilisha mazao na wakati wa kupalilia pandishia udongo kufunika mizizi.
· Karoti Kuwa na Mizizi Mingi (Folking);
Hii hutokea kama karoti zimepandwa kwenye udongo wenye takataka nyingi na usiolainishwa vizuri. Vile vile utumiaji wa mbolea za asili zisizooza vizuri unaweza kusababisba karoti kuwa na mizizi mingi. Hali hii inaweza kuzuiwa kwa kulainisha udongo vizuri na kutumia mbolea za asili zilizooza vizuri.
Mavuno
Karoti hukomaa siku 90 hadi 120 baada ya kupanda kutegemea na aina ya mbegu na hali ya hewa. Wastani wa mavuno kwa eka moja ni tani 10 au zaidi ambazo tani kumi hizi ni sawa na kilo 10,000 kwa eka moja.

ASANTE KWA KUFUATILIA BLOG YETU 
KARIBU KWA SOMO LINGINE SIKU NYINGINE 

Sunday, 21 August 2016

JINSI YA KUTENGENEZA CHAKULA BORA CHA KUKU WA KIENYEJI














Zifuatazo ni malighafi za kutengenezea chakula cha kuku wa kienyeji hapohapo nyumbani kwako;
1. mahindi 
2. pumba 
3. chokaa
4. damu
5. chumvi

TAZAMA JINSI YA KUTENGENEZA 
,,,,,,,,, 
-CHUKUA MAHINDI 50Kg HALAFU YAPARAZE,,,kuparaza ni kuvunja vunja punje za mahindi 
-PUMBA YA MAHINDI 5Kg
- MASHUDU YA PAMBA/ALZETI 5Kg
-DAGAA/VUMBI LA DAGAA 5Kg,,,Linapatikana sokoni 
- LIMESTONE (CHOKAA) 3Kg,,Inauzwa katika maduka ya pembejeo za Kilimo na Mifugo
- CHUMVI YA WASTANI NA MIFUPA UKIWEZA KUISAGA

WAWEZA CHANGANYA MCHANGANYIKO HUU KIASI CHOHOTE UNACHOWEZA ZINGATIA KANUNI ZILIZOTOLEWA HAPO JUU.

KUKU WA KIENYEJI WALIO FUGWA KATIKA MABANDA WAPE CHAKULA HIKI MARA TATU KWA SIKU KILA SIKU. LAKINI KWA KUKU WA KIENYEJI WANAOZURURA WAPE CHAKULA HIKI MARA MBILI KWA SIKU, ASUBUHI WAKATI WANATOKA KATIKA BANDA NA JIONI WAKATI WANARUDI KATIKA BANDA.

KAWAIDA YA KUKU WA KIENYEJI WAKATI WA KULA NI KUPARUA KWAHIO CHOMBO CHA KUWEKEA CHAKULA HIKI KIWE KIKUBWA KUZUIA KUMWAGA CHAKULA OVYO.

ASANTE MPENZI MSOMAJI WA BLOG HII KWA SOMO FUPI  ENDELEA KUTUFUATILIA TENA KWA AJILI YA KUPATA SEMINA NA MAFUNDISHO MBALIMBALI YA UJASIRIAMALI NA JINSI YA KUPAMBANA NA MAISHA NJE YA AJIRA.. 

KARIBU TENA

MWANDAAJI;;;MAGANGA J. ONGALA 
KWA KUSHIRIKIANA NA WATAALAM WA MIFUGO

Saturday, 20 August 2016

CHUKUA HATUA NJOO UONE VIVUTIO VILIVYOPO TANZANIA.....KARIBU




JE, UNAIFAHAMU HIFADHI YA TAIFA GOMBE?

NI HIFADHI YENYE WANYAMA SOKWE MTU IPO TANZANIA, WANYAMA HAWA SOKWE MTU (CHIMPANZEE) NDIYO WANYAMA WANAO KALIBIANA SANA NA BINADAMU. KUKALIBIANA HUKU NI KWA MUONEKANO WA NJE (PHENOTYPE) NA MUONEKANO WA NDANI (GENOTYPE)
IJUE ZAIDI HIFADHI HII PONYEZA HAPA. TUNZA MAZINGIRA ILITUENDELEE KUUFURAHIA ULITHI WETU..


Tunakuletea vitu orijino kutoka katika chanzo

UFUGAJI WA NYUKI ni shughuli zilizokuwepo tangu enzi na enzi, faida za ufugaji nyuki ni nyingi lakini kwa ufupi utajipatia kipato, utaboresha afya ya familia yako na hata kufikia malengo yako ya kuwa na nyumba nzuri, biashara yako nzuri (asali na nta),

kusomesha watoto na mengine mengi. ufugaji wa nyuki unakufanya utambulike Duniani. na mwisho ufugaji nyuki ni njia mbadala ya utunzaji mazingira.

NB; Kutakuwa na somo la ufugaji nyuki,,,endelea kutufuatilia ufikie malengo

Friday, 19 August 2016

Habari ndugu zangu, tutakuwa tuna badilishana mawazo kuhusu hifadhi za mazingira....

bila kusahau MAMBO YA KUZINGATIA WAKATI WA KUANZA UFUGAJI NYUKI KISASA
MPENZI MSOMAJI WA BLOG HII NZURI

TUTAKUWA TUNAENDESHA NA KUFUNDISHA MASOMO YA UFUGAJI NYUKI NA HIFADHI ENDELEVU YA MAZINGIRA