Karoti ni
zao ambalo hulimwa zaidi katika mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Morogoro, Iringa,
Mbeya na Kagera. Ndugu msomaji maeneo tajwa hapo juu hulimwa zaidi kwa maana
hiyo karoti inaweza kulimwa katika maeneo mengine pia yenye sifa zinazo
kalibiana na hiyo mikoa. hustawi vizuri kwenye sehemu zenye joto la wastani (nyuzi joto 15 hadi
27 za Sentigredi).
Zao hili hutumika kama kiungo katika mapishi ya vyakula
mbalimbali. Huweza kutafunwa mbichi au kuchanganywa kwenye kachumbari. Karoti
zina vitamin A, C na madini aina ya chuma.
Karoti hupandwa moja kwa moja shambani katika matuta au sesa.
Kiasi cha gramu 80 (sawa na vijiko vidogo vya chai 16) kinatosha kupanda eneo
la mita za mraba 100. Eka moja huhitaji kilo 3.2 za mbegu.
Hakikisha mbegu unazozipanda zina uwezo wa kuota kwa kuzifikicha.
Mbegu zenye uwezo wa kuota hutoa harufu kali unapozifikicha. Zilizopoteza uwezo
wa kuota huwa hazitoi harufu yoyote. Ili mbegu ziote haraka ziloweke katika
maji kwa muda wa saa 24. Baada ya hapo changanya mbegu hizo na mchanga, kwa
kiasi kinacholingana ili kupata mtawanyiko mzuri wa mbegu wakati wa
kupanda/kusia.
Maandalizi ya shamba
Ø
Lima
shamba kwa trekta, kwa ng’ombe ama kwa jembe la mkono kwa kina cha sentimita 30
hadi 45
Ø
Andaa
matuta yenye mwinuko na kimo cha sentimita 30-40, na upana wa mita 1 na mita
1.5 kutoka katikati ya tuta na tuta. Tengeneza mifereji midogo ya kusiha mbegu
za karoti yenye umbali wa sentimita 15- 20, mifereji minne kwa tuta
Ø
Weka
mbegu katika chupa ndogo ya mililita 100 na toboa kidogo mfuniko
Ø
Sia
mbegu katika mifereji ya kupandia kwa kutikisa chupa yenye mbegu
Ø
Funika
mbegu kwa kutumia mboji au mchanga
Ø
Nyunyiza
maji ya kutosha
Ø
Funika
tuta na plastiki nyeusi
Ø
Kandamiza
plastiki kwa pembeni na kwa mabonge ya udongo ili isipeperushwe na upepo
Ø
Mbegu
huota baada ya siku 3-5 kutegemea na hali ya hewa
Ø
Zingatia
kukagua shamba mara tatu kwa siku.
Ø
Ondoa
plastiki mara moja pindi utakapoona mbegu moja tu iliyoota
Ø
Kuchelewa
kuondoa plastiki husababisha miche inayoota kufa kwa kuunguzwa na joto lililo
katika plastiki
Palizi
Palilia shamba mara kwa
mara ili kuhakikisha shamba halina magugu
Magugu hudhibitiwa kwa
palizi ya jembe, kung’oa kwa mkono ama matumizi ya viuagugu
Matumizi ya viuatilifu
yafanyike kila baada ya wiki mbili
Mbolea
Tumia mbolea ya DAP
wakati wa kupanda, CAN ama SA wiki tatu baadaye na kisha tumia NPK wiki sita
baada ya kupanda. Matumizi ya mbolea za maji yafanyike kila baada ya wiki mbili
kutegemea na mahitaji
Magonjwa:
· Madoajani (Leaf Spot):
Ugonjwa huu husababishwa na ukungu na hutokea wakati karoti zina
urefu wa sentimita 13 mpaka 15. Hushambulia majani na kuyafanya yawe na madoa
yenye rangi nyeusi iliyochanganyika na kijivu au kahawia. Sehemu zinazozunguka
madoa haya hubadilika rangi na kuwa njano. Ugonjwa ukizidi majani hukauka. Zuia
ugonjwa huu kwa kunyunyizia dawa za ukungu kama vile Dithane-M 45, Blitox,
Copperhydroxide (Kocide), Copper Oxychloride, Cupric Hydroxide (Champion),
Antrocol, Topsin M- 70% na Ridomil.
· Kuoza Mizizi (Sclerotinia Rot).
Ugonjwa huu husababishwa na ukungu na hushambulia mizizi namajani.
Dalili zake ni kuoza kwa mizizi na majani. Baadaye sehemu hizi hufunikwa na
uyoga mweupe. Kwenye uyoga huu huota siklerotia kubwa zenye rangi nyeusi.
Zuia ugonjwa huu kwa kuzingatia yafuatayo:-
- Epuka kustawisha karoti kwenye maeneo yaliyoshambuliwa na
ugonjwa huu.
- Nyunyuzia dawa za ukungu kama vile Dithane M- 45, Blitox, Topsin
- M 70% na Ridomil.
· Madoa Meusi (Black Leaf Spot):
Huu pia ni ugonjwa wa ukungu unaoshambulia majani na mizizi.
Majani yaliyoshambuliwa huwa na rangi ya manjano ambayo baadaye hubadilika na
kuwa kahawia. Mizizi huwa na madoa meusi yaliyodidimia. Ugonjwa huu unaweza
kuzuiwa kwa kutumia mbegu zilizothibitishwa kitaalamu, kubadilisha mazao na
kuepuka kujeruhi karoti wakati wa kupalilia, kuvuna au kusafirisha.
Wadudu:
· Minyoo Fundo:
Minyoo hii hushambulia mizizi na kuifanya iwe na vinundu. Hali hii
husababisha mmea kudumaa na kupunguza mavuno. Minyoo fundo huweza kuzuiwa kwa
kubalidilisha mazao. Baada ya kuvuna usipande mazao yajamii ya karoti au mazao
yanayoshambuliwa na wadudu hawa. Unawezakupandamazao ambayo bayashambuliwi na
minyoo fundo kama vile mahindi. Pia hakikisha shamba ni safi wakati wote.
· Imi wa Karoti:
Mashambulizi hufanywa na funza ambaye hutoboa mizizi. Ili kuzuia
wadudu hawa tumia dawa kama vile Dichlorvos, Sapa Diazinon na Fenvalerate. Pia
badilisha mazao na wakati wa kupalilia pandishia udongo kufunika mizizi.
· Karoti Kuwa na Mizizi Mingi (Folking);
Hii hutokea kama karoti zimepandwa kwenye udongo wenye takataka
nyingi na usiolainishwa vizuri. Vile vile utumiaji wa mbolea za asili zisizooza
vizuri unaweza kusababisba karoti kuwa na mizizi mingi. Hali hii inaweza
kuzuiwa kwa kulainisha udongo vizuri na kutumia mbolea za asili zilizooza
vizuri.
Mavuno
Karoti hukomaa siku 90
hadi 120 baada ya kupanda kutegemea na aina ya mbegu na hali ya hewa. Wastani wa mavuno kwa eka moja ni tani 10
au zaidi ambazo tani kumi hizi ni sawa na kilo 10,000 kwa eka moja.
ASANTE KWA KUFUATILIA BLOG YETU
KARIBU KWA SOMO LINGINE SIKU NYINGINE